JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/E/34 17 Februari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).Pamoja na kazi zingine chombo hiki kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 517 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu tawala Mkoa Pwani, Katibu tawala Mkoa Simiyu, Katibu tawala Mkoa Katavi, Katibu tawala Mkoa Iringa, Katibu tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu tawala Mkoa Kagera, Katibu tawala Mkoa Rukwa na Katibu tawala Mkoa Njombe.
Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Nafasi hizi pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Arusha, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Tabora.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa kwa sharti hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji wanatakiwa kuambatisha maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Machi, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
xvi. Pamoja na waombaji kuainisha waajiri, Sekretarieti ya Ajira baada ya usaili itawapangia waombaji waliofaulu, kwa mwajiri yoyote bila kujali chaguo la mwombaji.Hii ni kutokana na baadhi ya waombaji kupendelea kufanya kazi kwenye baadhi ya maeneo tu.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.
1.0 AFISA LISHE II (NUTRITION OFFICER II) – NAFASI 21
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya taarifa na takwimu za lishe kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali na kutoa ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi ya wilaya.
Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa ya watoto na makundi mengine yenye lishe duni.
Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya lishe katika ngazi ya wilaya.
Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya lishe katika ngazi ya wilaya.
Kusimamia kazi za lishe katika wilaya
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajriwa wenye Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi na Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and Technology and Food Science) au Stashahada ya juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
2.0 MSAIDIZI LISHE (NUTRITION ASSISTANT) – NAFASI 16
2.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kutambua na kuorodhesha na kuweka kumbukumbu za watoto chini ya miaka mitano na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni ngazi ya kijiji na kata.
Kufuatilia na kutoa ushauri wa lishe kwa kaya zenye watoto wenye lishe duni.
Kuelekeza watoto na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni wapelekwe kwenye kituo cha afya Kwa huduma zaidi.
Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za lishe zinazotolewa kwa makundi mbalimbali kwenye kata/kijiji.
Kukusanya taarifa na takwimu za lishe katika sehemu yake ya kazi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye cheti cha miaka miwili cha mafunzo ya lishe kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS A kwa mwezi
3.0 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT)– NAFASI 12
3.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kulea watoto katika vituo vya malezi ya awali ya watoto wadogo mchana.
Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi bora ya awali ya watoto wadogo wenye umri wa miaka 0-8.
Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya watoto vijijini/sehemu au eneo la vituo.
Kuwa kiongozi wa kituo cha malezi ya awali ya watoto wadogo.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu mafunzo ya mwaka mmoja ya malezi ya awali ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0-8 kutoka katika Chuo kinachotambulika na serikali au wenye cheti cha mwaka mmoja cha mafunzo ya ustawi wa jamii.
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B Kwa mwezi
4.0 AFISA USTAWI WA JAMII II (SOCIAL WELFARE OFFICER II)– NAFASI 184
4.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kuendesha usaili kwa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, pamoja na watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali).
Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili.
Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa.
Kupokea na kukusanya taarifa za ustawi wa jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya ustawi wa jamii.
Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee malezi ya watoto na familia zenye matatizo.
Kupokea kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ambao (foster care) na vyuo vya malezi vya watoto wadogo mchana.
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja.
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali.
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.
Kuhoji na kuandaa taarifa za washtakiwa.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya B.A (social work or sociology) au stashada ya juu ya Ustawi wa jamii (Advanced Diploma in Sociol work) kutoka chuo cha juu kinachotambuliwa na ustawii wa jamii.
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
5.0 MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE ASSISTANT II) – NAFASI 24
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.
Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.
Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi.
6.0 MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II (KITCHEN/MESS ATTENDANT) – NAFASI 4
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusafisha Vyombo vya kupikia.
Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.
Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.
Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani.
Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.
Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne.
6.3 MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
7.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II) – NAFASI 6
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.
Kufanya utafiti wa misitu.
Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.
Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
Kukusanya takwimu za misitu.
Kufanya ukaguzi wa misitu.
Kupanga na kupima madaraja ya mbao.
Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.
Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya miti kwa wananchi.
Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
8.0 MSAIDIZI MISITU DARAJA LA II (FORESTRY ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 75
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya mbegu
Kuhudumia na kutunza bustani za miti.
Kutunza na kuhudumia miti na misitu.
Kufanya doria.
Kusimamia ukusanyaji mbegu na bustani za miti.
Kukusanya takwimu za misitu.
Kusimamia kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu.
Kukusanya maduhuli.
Kupima mazao ya misitu.
Kufanya doria.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B/C kwa mwezi.
9.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURE GENERAL) – NAFASI 10
9.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
9.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
10.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRONOMY) – NAFASI 4
10.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
10.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agronomy) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
11.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HORTICULTURE) – NAFASI 1
11.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
11.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Horticulture) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
12.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HUMAN NUTRITION) – NAFASI 1
12.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
12.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Human Nutrition) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
13.0 AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 71 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,
Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,
Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine,
Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,
Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,
Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
Kufanya utafiti mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,
Kufanya utafiti wa udongo,
Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,
Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,
Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
13.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
14.0 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 38 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,
Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,
Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na
Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.
15.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 2 (LINARUDIWA)
KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusaidia kuunda boti za uvuvi
Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
Kufanya matengenezo ya boti.
Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.
15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye stashahadaya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
15.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
16.0 DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II (FERRY / BOAT OPERATOR) – NAFASI 1 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
MAJUKUMU YA KAZI
Kufunga na kufungua kamba za kivuko.
Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.
Kupanga abiria au magari kwenye kivuko.
Kuendesha na kuongoza kivuko.
Kutunza daftari za safari ya kivuko.
Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
16.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.
16.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
17.0 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II) – NAFASI 8
(LINARUDIWA). KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.
Ataratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
Atasaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani.
Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
Atafanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.
Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
Atafuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo(Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana nayo.
17.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
18.0 MHASIBU MSAIDIZI (ASSISTANT ACCOUNTANT) - NAFASI 3
18.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kupokea na kulipa fedha.
Kutunza daftari ya fedha.
Kufanya usuluhisho wa hesabu za benki
Kukagua hati za malipo.
Kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha.
Kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu.
18.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha kufaulu mtihani mgumu wa Uhasibu Serikalini (Higher Standard Government Accountancy Examination) unaotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma. Au
Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyyote inayotambuliwa na serikali.
18.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi
19.0 AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
19.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja ( Jointy Venture )
Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishi katika vyama vya ushirika vya Msingi.
19.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika fani ya Ushirika (Cooperative management and accounting) kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
19.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
20.0 AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
20.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa makisio ya vifaa vinavyohitajika (Material Requirement Budget) na Mpango wa Ununuzi (Procurement Plan).
Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji za Wazabuni mbalimbali.
Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji, na usambazaji wa vifaa.
Kusimamia utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical Distribution).
Mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design).
Kusimamia ukaguzi wa kuhesabu vifaa mara kwa mara (Perpetual Stock Checking) ghalani.
Kutayarisha Taarifa za kazi katika vipindi maalumu.
Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kila mwisho wa mwaka (Annual Stock Taking).
Kufanya kazi zingine ambazo atapangiwa.
20.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara (B.Comm) yenye mchepuo wa ugavi au Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advanced Diploma in Materials Management) inayotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya usimamizi wa Vifaa.
20.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D mwezi.
21.0 AFISA UGAVI MSAIDIZI II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER) – NAFASI 1
21.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.
Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.
Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.
Kufungua “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.
Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.
Kuandaa hati za kupokelea vifaa.
Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
21.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha “National Store-Keeping Certificate au “Foundation Certificate” kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
AU
Kuajiriwa wenye Diploma ya Kawaida “Ordinary Diploma in Materials Management” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
21.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.A na B kwa mwezi.
22.0 AFISA UTAMADUNI II (CULTURAL OFFICER GRRADE II) – NAFASI 1
22.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutafiti masuala ya Lugha, Sanaa, Mila na Desturi katika ngazi ya Wilaya.
Kufundisha fani mbalimbali za utamaduni katika Vyuo na Vituo vya Elimu na mafunzo ya utamaduni.
Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.
22.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada au stashahada ya juu katika Sanaa, Lugha au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.
22.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
23.0 AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
23.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuratibu na kisimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana
Kuratibu shughuli za mikopo/mifuko ya Vijana
Kuhamasisha vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini
Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya Vijana
Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, Ajira kwa Vijana na Elimu ya Familia kwa kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali (NGO)
Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu Vijana
Kuratibu shughuli mbalimbali za NGO zinazoshughulikia masuala ya Vijana
Kuandaa mipango ya kuboresha malezi ya Vijana
Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali
Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo Vijana ili kuwawezesha kujiajiri
Kuandaa mipango ya kuwahamasisha Vijana ili kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiajiri.
23.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (BA. in Sociology or Social Sciences) au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii au Ustawi wa Jamii au Maendeleo ya Vijana (Advanced Diploma in Social Works or Community Development or Youth Development) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serkali.
23.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
24.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
24.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.
Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
24.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
24.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
25.0 AFISA ARDHI DARAJA LA II (LAND OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
25.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia uingizaji wa kumbukumbu katika kompyuta.
Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria.
Kufanya ukaguzi wa viwanja.
Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki kwa visivyoendelezwa kwa mujibu wa sheria.
Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi.
25.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Usimamizi ardhi na Uthamini au Shahada ya Sheria kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitano.
25.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi
26.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - KOMPYUTA (COMPUTER TECHNICIAN GRADE II) – NAFASI 1
26.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
26.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani yenye muelekeo wa kompyuta
Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya kompyuta
Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani yenye muelekeo wa kompyuta katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
26.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
27.0 AFISA BIASHARA DARAJA LA II (TRADE OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
27.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuwasiliana na Wizara nyingine ambazo zinafanya biashara, kupata takwimu ambazo zitatumika katika kutathimini mwenendo wa biashara na masuala mengine ya kibiashara.
Kusambaza taarifa za kibiashara kwa wafanyabiashara.
Kutathmini mwenendo wa biashara kwa kuangalia hali ya masoko katika nchi mbalimbali ambazo bidhaa zetu zinauzwa.
Kuandaa grafu na “chart” ambazo zinaonyesha, mwenendo wa bidhaa zinazoingizwa nchini na zile ziendazo nje kwa kila nchi ambazo hufanya biashara na Tanzania.
27.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Biashara waliojiimarisha katika fani ya Uchumi, Masoko, Uendeshaji Biashara au inayolingana nayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.
27.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
28.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 1
28.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.
Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
28.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA
28.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
29.0 AFISA USIMAMIZI WA FEDHA DARAJA LA II (FINANCE MANAGEMENT OFFICER II) - NAFASI 1
29.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandikisha na kudhibiti Amana (Securities) za Serikali.
Kufuatilia hati za hisa.
Kuwasiliana na watoaji mikopo/misaada kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi.
Kuweka kumbukumbu za madeni ya nje.
Kuweka kumbukumbu za mikopo ya ndani.
Kufuatilia na kusimamia matayarisho ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali.
Kufuatilia utayarishaji na uchambuzi wa “Flash Reports” za kila mwezi.
29.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Uchumi na Mipango (Major in Economics) au Biashara au Sheria (LL.B) au Stashahada ya Juu ya Uhasibu au Uchumi & Mipango au Biashara au Stashahada ya juu ya Usimamizi wa kodi kutoka Chuo/Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
Waombaji wenye Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na NBAA watafikiriwa kwanza.
29.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
30.0 AFISA TARAFA – NAFASI 6
30.1 MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.
Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.
Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake
Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.
30.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Sheria,Menejimenti,Utawala,Sayansi ya Jamii, Kilimo, Mifugo,Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
30.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.
31.0 AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
31.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa vyuo, shule, na vituo vya Elimu na Mafunzo
Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa waalimu, Makocha, viongozi wa vyama na vilabu vya michezo
Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.
31.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo (Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
31.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
32.0 FUNDI SANIFU DARAJA II – RAMANI (TECHNICIAN GRADE II - (MAPPING) – NAFASI 1
32.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kushughulikia madaai/malalamiko ya hati za viwanja, kuweka na kutunza kumbukumbu zake
Kutunza kumbukumbu za “cadastrals surveys” na mahesabu yake
Kuandaa nakala za “cadastral site plans”
Kutunza miongozo ya ramani (maping guides) na viwanja
32.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ramani (Mapping)
32.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
33.0 FUNDI SANIFU DARAJA II- URASIMU RAMANI (CARTOGRAPHY) – NAFASI 1
33.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya maandalizi ya Uchoraji wa ramani za miji kadiri ya uwiano unaohitajika
Kutunza kumbukumbu za ramani na plan
Kuchora plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji
Kutoa nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji
33.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili au Stashahada katika fani ya Urasimu Ramani (Cartography) kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
33.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
34.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI - (TECHNICIAN GRADE II - WATER) – NAFASI 1
34.1 MAJUKUMU YA KAZI
Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji
Kutunza takwimu za maji
Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro
Kuchora hydrograph za maji
Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post” n.k.
Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa
Kuingiza takwimu kwenye kompyuta
Kufundisha wasoma vipimo
34.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
34.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
35.0 AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 1
35.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutekeleza Kazi za Ushirikishaji Wadau Katika Uhifadhi.
Kudhibiti Utoaji wa Leseni za Biashara Za Nyara na Vibari vya Kukamata Wanyama Hai.
Kushiriki Katika Kusuluhisha Migogoro ya Matumizi ya Wanyamapori
Kudhibiti Matumizi Haramu ya Leseni za Uwindaji na Kuhahakikisha Kufuatwa Kwa Maadili Katika Kutumia Wanyamapori.
Kuthibiti Matumizi Haramu ya Wanyamapori.
Kufuatilia Utekelezaji wa Miongozo Mbalimbali ya Uhifadhi Wanyamapori.
Kuhakiki Viwango vya Kukamata Wanyama Hai Kwa Ajili ya Biashara na Ufugaji.
Kufanya Kazi za Kuzuia Ujangili.
Kukusanya Taarifa, na Takwimu za Uhifadhi.
Kutekeleza Kazi za Uhifadhi Katika Mapori ya Akiba.
35.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori Kutoka Chuo Kikuu Kinachotambuliwa na Serikali.
35.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi
36.0 AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) – NAFASI 2
36.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni pamoja na:
Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.
Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.
36.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
36.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi
X. M. Daudi
Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
The blog is intended to provide the readers daily news on Tanzania politics,Tourism, education , Business, health, culture, sports, artwork, family/friend affairs, travel, social welfare, community dev, general knowledge and life ventures. Welcome
Friday, 28 February 2014
Friday, 7 February 2014
Employement Opportunity
Africare is
searching for a qualified person to fill the position of Director of Finance
for a USAID funded nutrition program under Feed the Future. The position will
report to the Chief of Party on the implementation of the program. The Director
of Finance will oversee all the financial issues and advice the CoP
accordingly.
Key Responsibilities
1.0
Program
Funds Management
1.1
In coordination with Chief of Party, prepare Quarterly
Funds Requests (to be submitted to CO), ensuring that the minimum amount of
funds are available in-country to fully implement projects and meet all
Africare’s financial engagements in timely manner.
1.2
Prepare periodic cash flow projections for the project
as required by Africare CO.
1.3
Maintain financial and accounting systems and reporting
as guided by the rules and regulations of USAID and Africare.
1.4
Review all invoices and payments to ascertain
compliance with Africare procedures including availability of funds before
seeking COP and Country Director approval.
1.5
Perform periodic reviews and certify the General
Ledger, cash book, Trial balance and other pertinent reports generated in
Financial accounting system by the 15th of every month in time for
monthly batch dispatch to CO.
1.6
Maintain Accounts Receivable (A/R) for all program
staff and ensure settlement of all cash advances within specified timeframe as
per financial manual.
1.7
Prepare financial reports as per donor requirements and
timeline with in addition to Africare financial formats
2.0
Budgeting
and Reporting
2.1
Develop project’s Annual Operating budgets as per donor
agreement and Africare guidelines.
2.2
Develop and maintain budgetary controls of expenses, in
consultation with Chief of Party and Program staff.
2.3
Prepare donor billings and financial reports and submit
to donors within the agreed schedules.
3.0
Grants
Management and facilitation of Audits
3.1
Oversee the facilitation and management of the
sub-grant making process through Grants Manager as per Africare Grants manual,
in tandem with donors’ rules and regulations on financial management.
3.2
Prepare and
facilitate external audits as appropriate in consultation with donor
requirements
4.0
General
Administration
4.1
Ensure that adequate internal controls and procedures
are in place, understood and adhered to.
4.2
Remain up-to-date on Government of Tanzania and
Government of United States financial management and reporting requirements.
4.3
Oversee the maintenance of an assets register.
4.4
Supervises and coordinate the work and assignments
performed by the field staff including allocation and/or review of duties as
appropriate from time to time.
5.0
Procurement
of Goods and Services
5.1
Work closely with project’s Procurement/Logistics
office to ensure procedures are complied with as specified in Africare
procurement policy for goods and services.
5.2
Maintain service agreements with Africare
contractors/providers of goods and services.
6.0
Representation
6.1
As a member of the Project’s senior management team,
maintain good relations with Africare stakeholders including Donors,
Government, collaborating partners and communities, adequately espousing
Africare principles at all times.
Observe
the functions of the positions as one of the “key personnel” listed in the
donor grants agreements
Qualification and competencies:
·
A degree or postgraduate qualification in
accounting and finance.
·
CPA holder
·
Experience in managing USAID funded projects is
a MUST
Personal Attributes:
In addition to
the above skills and qualifications, applicants are required to have the
following attributes:-
·
A very high level of integrity, honesty and
sense of responsibility.
·
Ability to work under pressure and produce
expected results.
·
Ability to work in a dynamic team.
·
Ability to self manage, achieve results and meet
deadlines.
·
Willingness to work beyond the call of duty
Skills and experience
·
Minimum of 5 years experience as a Senior
Accountant or Finance manager preferably in the international donors.
·
Experience with the NGO sector as well as
handling a diverse portfolio of funds from International donors.
·
Conversant with computerized accounting packages
including data presentation, Excel,QUICKBOOK and MS Word.
·
Proven strong analytical and problem solving
capabilities.
·
Must have excellent coordination, organizational
and inter – personal skills.
How to Apply
Applications
should include a resume and cover letter. In the cover letter (of no more than
two pages in length) the candidate should briefly describe his or her motivation
for the position and highlight relevant experience. Please include
"DIRECTOR OF Finance –
Nutritional Project." in the subject
line.
All applications should be sent
by email, Post or hand delivered to:
Human Resources Manager
Africare Tanzania
P.O.Box 63187
Dar es Salaam
Email: tanzania.vacancies@africare.org
The position and advert remain open until filled. Unfortunately,
due to the large number of applications that we receive, we may not be
able to respond to each individual candidate.
Please respect our no phone calls policy.
Thursday, 6 February 2014
SAID ISSA MOHAMED: Sitta alikuwa agombee urais CHADEMA 2010
Majibu kwa wanaodai Dr. Slaa alilazimisha mshahara mkubwa CHADEMA
SAFU yetu ya Mwanasiasa wa Wiki leo imebahatika kufanya mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa upande wa Zanzibar, Saidi Issa Mohamed, muda mfupi kabla hajapanda ndege kwenda nje ya nchi kwa shughuli za chama.
Miongoni mwa mambo anayoelezea Mohamed ni pamoja na namna walivyompata mgombea wa nafasi ya urais mwaka 2010 na suala zima la udini, ukanda na ukabila unaodaiwa kuwamo ndani ya chama chake.
Swali: Unazungumziaje suala la chama chenu kudaiwa kuwa na udini, ukabila na ukanda? Dini yenyewe inayozugumzwa ikiwa ni Ukristo wa madhehebu ya Katoliki na inasemekana mmewekwa pale kwa ajili ya kuficha madai hayo?
Mohamed: Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukuongoza kuniuliza hayo, hapo kuna maswali matatu, nitakujibu kila swali kwa nafasi yake, nikianza na suala zima la udini.
Kama watu wanafuatilia historia ya kuanzishwa kwa vyama vingi na wakaamua kukataa propaganda zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali nzima basi watabaini kuwa hakuna kitu kama hicho kwa Tanzania, ila waliofilisika kisera wanataka kutumia turufu hiyo ya udini kama nafasi ya kuonewa huruma katika jamii.
Nasema hivyo kwa sababu mtiririko mzima wa uongozi ndani ya CHADEMA, kuanzia kuasisiwa kwake haukuwa wa kuangalia dini bali uwezo wa mtu, na katika hili linadhihirishwa na namna uongozi ulivyokuwa tangu mwanzo hadi sasa, mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA alikuwa mzee Edwin Mtei.
Huyu ni Mkristo na katibu mkuu alikuwa mzee Ally Nyanga Makani ‘Bob Makani’, huyu ni Mwislamu, naibu wake kwa Bara alikuwa mzee Saidi Arfi, naye huyu ni Mwislamu na kwa viongozi waliotoka Zanzibar wote walikuwa Waislamu.
Awamu ya pili, mwenyekiti alikuwa Bob Makani, makamu Dk. Willbrod Slaa na katibu mkuu alikuwa Amani Walid Kabourou.
Awamu ya tatu, mwenyekiti wetu alikuwa Freeman Mbowe, makamu Kabourou, katibu mkuu, Dk. Slaa, katika nafasi ya makamu mwenyekiti hapa alikuwa Shaibu Akwilombe na baadae akawa Chacha Wangwe (marehemu).
Awamu hii tunayokwenda nayo sasa, Mbowe ameendelea kuwa Mwenyekiti, Makamu wake Bara ni Said Arfi, Zanzibar ni mimi, Katibu Mkuu ni Dk. Slaa, Naibu wake Bara ni Zitto Kabwe na Zanzibar ni Hamad Yusuph, hapa utaniambia Ukristo na huo Ukatoliki uko wapi?
Pia ukiangalia namna viongozi walivyo kuanzia mwanzo, hakuna safu nzima ya viongozi wakuu waliotoka kanda moja au kabila moja.
Kama kungekuwa na udini katika CHADEMA huo unaosemwa, basi Waislamu wasingepita na kuwa katika nafasi walizonazo leo, kwa kuwa nafasi zote za juu ni za kupigiwa kura.
Swali: Sasa unafikiri kwanini mambo hayo yanazungumzwa kuhusu ninyi na si vyama vingine?
Mohamed: Sasa hivi CHADEMA tupo katika mioyo ya watu na hili ni tishio kwa chama tawala, kama utakumbuka wakati ule CUF ilipokuwa juu waliambiwa ni chama cha kigaidi, cha Waislamu na mwisho kikaitwa cha Wapemba, nao walikubaliana na propaganda hizo pasipo kujua kuwa zinawamaliza, unaona leo wameshuka wale waliowazushia hawaoni tishio la CUF tena, sasa wameivamia CHADEMA.
Hii ni baada ya kutangazwa Kwa Dk. Slaa kuwa mgombea wetu mwaka 2010, lengo lilikuwa kuwagawa wananchi na kisha wawatawale, serikali inafanya hivi makusudi kwa kutumia idara zake za usalama ambao hawataki kutambua kuwa wapo kwa ajili ya masilahi ya taifa na si chama cha siasa.
Watanzania wanapaswa wajiulize kama CHADEMA kinasemwa ni cha Wakristo, CUF ya Waislamu na CCM itakuwa ya dini gani? Au hao wenye dini hizo zinazotajwa kuwa ni za CUF na CHADEMA wanajipendekeza ndani ya CCM?
Swali: Umehusisha idara za usalama kushiriki katika propaganda hizi na wao wanashiriki vipi? Wakati taarifa za chama hicho kuwa cha kidini zilikuwa zinatolewa katika nyumba za ibada?
Mohamed: Fahamu kuwa idara ya usalama ina watu wengi katika maeneo tofauti ya kijamii, hili la kusemwa kanisani au msikitini lisikupe taabu, kwani hata huko wana watu wao na ndio wanaokuwa wa kwanza kupokea tamko la uchonganishi kutoka katika dini nyingine na kulifikisha kwa waumini wao, katika mtazamo wa kawaida unaweza ukasema ni Wakristo au Waislamu ndio wamesema kumbe hilo limefanywa na watu waliokaa meza moja na kutengeneza ajenda ya kuwagawa Watanzania.
Sitaki kuwa mtabiri juu ya hili la kuwagawa watu kiimani kwa ajili ya kutaka kuungwa mkono katika uchaguzi, ni wazi sasa hata waliolianzisha limewashinda, imekuwa ni silaha ambayo mtaalamu wake ameshakufa na waliobaki hawana ujuzi wa kulifanya lisilete madhara. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Watanzania wasifikie katika hali ya kushikana mashati kwa ajili ya imani zao.
Swali: Kwanini unakataa kuwapo kwa suala la udini, ukanda na ukabila ndani ya CHADEMA wakati wapinzani wenu wanalihusisha hilo na namna mlivyowapata wabunge wa viti maalumu? Kwani idadi kubwa inaonekana kutoka Kanda ya Kaskazini, hili huoni kama linadhihirisha suala zima la ukanda na ukabila?
Mohamed: Binafsi kabla ya kuja CHADEMA nilikuwa mwanachama wa CUF, ninajua namna viti maalumu vinavyopatikana na huu utaratibu uliotumiwa na chama changu baada ya kuharibika uchaguzi mkuu wa baraza la wanawake ninasema ni mzuri na hauna tatizo lolote.
Swali: Mzuri vipi? Unaweza kunifafanulia huo uzuri unaousema na kuondoa shaka iliyojengeka kuwa nafasi zilikuwa za kupeana?
Mohamed: Tuliweka vigezo zaidi ya sita ambavyo havikuangalia imani ya mtu wala ni wapi mtu anatoka na kila kigezo kilikuwa na alama zake, hivyo waliofanikiwa kuwazidi wenzao kwa hivyo vigezo ndio walikuwa katika nafasi nzuri ya kuingia katika viti maalumu; navyo ni elimu, uzoefu wa aina yoyote katika kuitumikia jamii, mchango wa mhusika katika chama hapa ni wa hali na mali, na muda aliojiunga. Hivi ni kwa uchache, lakini nikuhakikishie hata wale waliokuwa ni makada wasaidizi waliweza kuongeza alama zao kwa uzoefu huo na wengine leo ni wabunge kupitia vigezo hivyo.
Swali: Tayari Tanzania imeshafanya uchaguzi mkuu wa wabunge na rais katika vipindi vinne, ambapo vyama vya upinzani vilishiriki na ninyi ndani ya CHADEMA mmeshiriki katika awamu zote hizo na kusimamisha wagombea wa urais mara mbili, je, mwanzoni hakukuwa na watu wa kuweza kugombea nafasi hizo?
Mohamed: Mwaka 1995 tulimuunga mkono mgombea wa urais kutoka chama kimoja kilichokuwa na nguvu wakati huo, mwaka 2000 ilikuwa tusimamishe mgombea wa nafasi ya urais na alikuwa ni mwanamke, cha kutusikitisha dakika za mwisho tuliyemtegemea akaamua kuachana na nia hiyo, mwaka 2005 mtakumbuka kulikuwa na mvutano mkubwa wa kuwania nafasi ndani ya CCM, nasi tulimuandaa Profesa Mwesiga Baregu, lakini mpaka dakika za mwisho sekretarieti ikawa haina taarifa zake na hata alipopatikana hakuwa tayari kugombea vile vile, tukaamua kumweka Mbowe, hakutaka, ila tulimlazimisha kwa ajili ya kukiweka chama mioyoni mwa watu, naye alikubali na akaachana na nia ya kugombea ubunge kule Hai.
Swali: Niambie namna mlivyompata Dk. Willibrod Slaa kuwa mgombea wenu na kuna madai kuwa aliwapa sharti la kumlipa mshahara anaoupata katika ubunge endapo angekosa nafasi ya urais mwaka 2010?
Mohamed: Kwanza nikurejeshe kidogo katika harakati za kumpata mgombea wa chama chetu mwaka 2010, kwa asilimia kubwa tulijua Samuel Sitta angesimama kwa ajili ya CHADEMA na mawasiliano hayo tulikuwa nayo hadi muda unakaribia wa kupeleka majina ya wagombea, lakini Sitta akatugeuka dakika za mwisho. Hii inaonesha namna ndani ya CHADEMA tusivyokuwa na tamaa ya kugombea urais bali tunataka ufanisi.
Baada ya Sitta kutugeuka tukasema tunao watu wetu, tena ni wazuri na wanaaminiwa na wananchi, vijana na wasomi mbalimbali wakaingia mikoani kufanya utafiti ni nani anaweza kusimama kwa ajili ya CHADEMA, jibu likaja kuwa ni Dk. Slaa.
Ugumu ukawa namna ya kumshawishi aachane na ubunge, kwa kuwa alikuwa amekwisha kuchukua hadi fomu kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu. Tulijadiliana wenyewe kwanza kabla ya kumwambia kuwa kamati kuu itamteua, na Mwenyekiti Mbowe alifanya hili kuwa siri kubwa kwa Dk. Slaa na hapo ndipo tulipomshitukiza.
Baada ya kumshitukiza Dk. Slaa kama unavyomjua, kwanza alishangaa na hakuwa na jibu la kusema. Lakini nikuambie, hapa kulitokea mtafaruku. Mjumbe wa kamati kuu, huyu bwana anaitwa, Maasey, anatoka Karatu, alisimama kwa ghadhabu na kuuliza, kwanini katika hili hatujawashirikisha watu wa jimbo lake. Kwa kweli ulikuwa mtafaruku, hadi akasema kama tumeamua kumfanya Dk. Slaa kuwa mgombea urais wa CHADEMA, wao Karatu wanahamia CCM.
Hii yote ni kwa mapenzi na uwajibikaji wa Dk. Slaa, ndiyo maana kila mmoja akataka kuwa karibu yake. Kiutendaji wao Karatu waliona wanampoteza mchapakazi katika jimbo lao, lakini tuliwafahamisha kuwa kwa masilahi ya nchi na chama ni vema wakubaliane na uamuzi wa kamati kuu.
Suala likaja, je, kama atashindwa tutamuwajibikia vipi? Napo tukakaa chini na kufanya tathmini kuwa huyu kwa Karatu anapita kwa asilimia 100 na kama ikitokea akashindwa katika nafasi ya urais, basi tumlipe mshahara wa ubunge. Haya ni makubaliano ya wote, si kwamba Dk. Slaa alilazimisha.
Baada ya kujadiliana hili kwa pamoja ikatulazimu kuunda timu ya kwenda Karatu kuwaelezea umuhimu wa wao kumwachia Dk. Slaa kuwa kinara wa kuivusha CHADEMA katika hatua iliyokuwapo, nao wakatuelewa na wakatuahidi jimbo hawatalirudisha kwa CCM, kweli walitimiza ahadi yao, watu wale ni waaminifu katika ahadi zao.
Monday, 3 February 2014
Mchungaji Mtikila anusurika kuuawa
Kiongozi wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amenusurika kifo na mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Mikidadi, ambaye yupo mahututi katika Hospitali ya Temeke, baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na mzozo wa ardhi eneo la Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Mtikila alikumbwa na mkasa huo Ijumaa wiki iliyopita baada ya kufika katika eneo hilo kwa nia ya kutaka kuwaondoa watu hao wa familia tatu tofauti ambao wanaishi katika eneo hilo.
Kipigo hicho ambacho kimemsababishia majeraha ya kisogoni na hata kushonwa nyuzi tatu kichwani, kuvimba usoni na maumivu makali mwilini yalitokana na kipigo kutoka kwa familia mbili tofauti zinazoishi katika eneo hilo ambao wanapinga kuhama.
Pia katika sakata hilo, Mtikila anadai kupoteza simu mbili, pesa taslimu Sh400,000 na Dola za Marekani 2,000 na siku ya tukio na alifika hapo akiwa ameongozana na watendaji wa Dawati la Msaada wa Kisheria katika taasisi yake ya Liberty Fund International.
Kamanda wa Polisi Temeke, Engbert Kiondo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanalifanyia uchunguzi na taarifa kamili itatolewa kesho Jumanne.
"Ni kweli suala hilo limeripotiwa hapa na tunalifanyia uchunguzi na kesho Jumanne nitatoa taarifa rasmi kwa waandishi wa habari," alisema Kiondo.
Mtikila alisema, mara baada ya kufika eneo hilo, alikwenda katika nyumba ya kwanza na kuwakuta walinzi ambao walikubali na kuondoka katika eneo hilo kwani tayari notisi walikuwa nayo na walikuwa wanatambua kuwa wanatakiwa kuondoka.Alisema baadaye walikwenda katika nyumba ya pili ambayo anaishi mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Rubein Sanga ambaye hata hivyo vitu vyake vingi akuwa amekwisha vihamisha.
Alisema wakiwa mbele ya nyumba hiyo gari la polisi lilifika na wakiwa hawana hili wala lile vijana ambao anawataja kuwa ni wa Sanga walianza kuwashambulia kwa kutumia nondo na kila aina ya silaha za jadi.
"Walinipiga sana hadi nikapoteza fahamu na wakawa wanasema huyo Mtikila bebeni na mumchome moto, walitaka kuniua kwani walinikwida tai hadi ikakatika," alisema.
Na kuitaja pia familia ya Evelyne Mboya kuwa ilishiriki kuwashambulia. Alisema wakati vurugu zinaendelea, ndipo akatokea mmoja wa jirani wanaoishi katika eneo hilo aliyemtaja kwa jina la Mikidaki: "Yule bwana alipojaribu kunitetea kuwa nisiendelee kupigwa alipigwa nondo kichwani na akaanguka na alishambuliwa hadi kuzirai na hajapata fahamu hadi leo," alisema.
Mchungaji Mtikila alisema alikuwa ameambatana pia na walinzi wawili (mabaunsa), wafanyakazi wa dawati lake la msaada wa kisheria lililopo chini ya taasisi yake ya Liberty Fund International na mmiliki halali wa eneo hilo, Omar Salum Muhsin ambaye pia alijeruhiwa mkononi kwa nondo.
Mtikila aliwataja wafanyakazi wake waliojeruhiwa kuwa ni Hemed Wendo na Gray Mhando na akiwa amezirai alibebwa na kupandishwa katika gari hadi Kituo cha Polisi Chang'ombe ambako yeye na wenzake walifunguliwa jalada kwa shtaka la kuingia isivyo halali katika eneo la watu wengine.
Subscribe to:
Posts (Atom)