Habari vijana wenzangu,
Nategemea kupeleka HOJA BINAFSI BUNGE LA 26 AUGUST 2013 KUHUSU AJIRA KWA VIJANA.
HINTS,
× Kuitaka Serikali iitishe sensa ya wahitimu wote wa fani zote na ifanye uchambuzi wa ikama ya utumishi katika wizara, idara, mikoa, halmashauri- serikali za mitaa, na mashirika yake ya Umma. Lengo ni kujua idadi ya wahitimu wasio na kazi na nafasi zilizowazi.
Utafiti wangu ni kwamba KWA UPANDE WA SERIKALI;
(A) KILA OFISI ya serikali INASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ipasavyo KWA AJILI YA UPUNGUFU WA WATUMISHI, HAKUNA OFISI IMETIMIA WATUMISHI
(B) KUNA WATU WENGI SANA WANAKAIMU NAFASI MPK WENGENE WANAKAIMU NAFASI ZILIZOKUWA ZINAKAIMIWA yaani KAIMU KAIMU AFISA UTUMISHI NK NA NAFASI YAKE HIVYO HIZI NI tatu nafasi kwa mtu mmoja
(C) KUNA WATU wanapewa ajira za mikataba na WANAONGEZEWA MIKATABA KWA KIGEZO KUWA HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUZIBA NAFASI HIYO au hakuna mwenye uzoefu. KWA UPANDE WA PILI SASA WA WAHITIMU;
(1) KILA MTAA KUNA KIJANA AU VIJANA WAHITIMU WANA MIAKA 2 HADI 5 HAWANA KAZI WANAZUNGUKA NA BAHASHA MPAKA SOLI ZA VIATU ZINAKWENDA UPANDE
(2) KILA MTAA VIJANA WAPO WAKIOMBA KAZI WANAAMBIWA HAWANA UZOEFU wa 2 or 3 yrs, Au anayetakiwa awe na 4yrs experience hata katika ngazi za ofisa wa ngazi za kuanzia ilihali hakuna chuo kinafundisha uzoefu
(3) Vijana wapo na diploma hawajulikani walipo kwa Serikali na wamekaa miaka 2 hadi 5 na diploma zao wanasubiri kazi. kipindi ambacho angewezeshwa kwenda shule angeshavuka diploma na degree angekuwa hata na master.
Kufuatia hali hii:
(i) vijana wanaitwa bomu ili hali VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA
(ii) Vijana wana stress, wamekata tamaa hawaoni future na wengine wanahasira sana
(iii) Vijana wahitimu wanatunzwa na wazee ambao hawakwenda shule hivyo kuwa mzigo kwa wazazi.
Lengo ni kuitaka serikali ikishajua idadi ya wahitimu na ikama yake cos ofisi ziko wazi mlioko ofisini mkisema ukweli msiogope mabosi wenu mtakiri hili
(1) Serikali ifanye re allocation ya vijana kwenye nafasi za kazi kufuatana na ujuzi wao,
(2) Serikali ianze kufanya attachment kwa vijana wapate uzoefu maofisini na hata kuwalipa half a saraly of a full employed officer ili kuondokana na tatizo la kukosa uzoefu kwa kijana aombapo kazi.
(3) Vijana wawe tayari kujitolea kulipwa hata half a saraly ili wapate uzoefu
(4) Uwezo wa kazi na marks za kwenye vyeti ni vitu viwili tofauti, serikali ikiwa attach ofisini vijana itajua uwezo wao itaacha kuongezea wastaafu mikataba kwa vigezo kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo
(5) Serikali ibane matumizi yake ili itenge fedha ya kuendeleza wahitimu. Mtu mwenye diploma kusubiri kazi miaka 5 ni kipindi angeweza kuwa na degree na masters yake. Baadhi sehemu za kukata matumizi ya serikali bila kuathiri kazi za serikali ni kwenye magari na mafuta ya magari.
Unakuta bosi anakaa bunju halafu dreva gongolamboto halafu ofisi posta, au bosi kiluvya dreva mbagala ofisi posta kila siku trip hizo, pia training nje ya nchi kwa mtu mwenye 59yrs nakutumia milions and milions zisitishwe ili tuandae generetion ya kupokea majukumu. Pia serikali ikishajua waliopo pia iandae projection ya tunakoelekea in three to five yrs hali itakuwaje na serikali inampango gani. Sababu maisha bora yanaletwa na KAZI.
SERIKALI IKISHAJUA IWEKE BAJETI AMA YA GUARANTEE AU YA KUFUFUA VIWANDA VYOTE VILIVYO LABOUR INTENSIVE ili kuchukua vijana wahitimu na wa mtaani. SENSA HII SIO GHARAMA NI KUWATANGAZIA TU WAHITIMU WAKAJIANDIKISHE KTK OFISI ILIOKARIBU AU KUPELEKA CV kwa DC the cv zinachambuliwa.
This is a rough idear. You can add or improve. VIjanaaaaaaaa, itikieni NGUVU KAZI YA TAIFA.
The blog is intended to provide the readers daily news on Tanzania politics,Tourism, education , Business, health, culture, sports, artwork, family/friend affairs, travel, social welfare, community dev, general knowledge and life ventures. Welcome
Sunday, 4 August 2013
Mwigulu Nchemba: Nategemea kupeleka hii Hoja yangu binafsi Bunge la August 2013 kuhusu Ajira kwa Vijana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment