Pages

Monday, 23 September 2013

WAVUNJA KANISA KATOLIKI NA KUACHIA HAJA KUBWA MADHABAHUNI HUKO PWANI

Watu wasiofahamika wameiba vitu kadhaa Kanisa Katoliki kigango cha Jaribu mkoani Pwani. 

Katekista wa kanisa hilo katoliki Joseph Mwiru kutoka Pwani anaeleza kuwa sanamu ya Bikira Maria, Msalaba, meza ya kusalia, na meza ya kuandalia vifaa, na kisha baada ya hapo kujisaidia haja kubwa sehemu tatu tofauti madhabahuni.

Katekista huyo anaeleza kuwa kuna baada ya kufuatilia walikuta vifaa vingine ambavyo vimetelekezwa maporini. Akihojiwa na Anthon Joseph wa kituo cha redio cha WAPO Radio FM kupitia kipindi cha uchambuzi wa habari wa Patapata, Katekista Joseph anasema kuwa wanachodani ni kwamba mtu/watu hao walifanikiwa kuingia baada ya lango la kanisa kuvunjwa kwa kutumia kitu kizito, ambapo inadhaniwa kuwa ni mojawapo ya tofali ambalo walikuwa wanaandaa ujenzi.

Katika kuelezea zaidi, imefahamika kuwa watu ama mtu huyo hakuja na kinyesi kwenye mfuko, bali walifanya kitendo hicho hapohapo, kutokana na muonekano wa taka ulivyokuwa. Haijajulikana hasa lengo ni kukomoa ama alikuwa na maana gani hasa kuachilia haja kubwa madhabahuni.

Afisa Mtendaji Kata; Rajabu Unga Mwipi anasema kuwa wamefika eneo la tukio na kushuhudia kweli kuwa pamevunjwa na meza mblii zimeibiwa huku baadhi ya picha zikitawanywa tawanywa, na vitu kadhaa vikikosekana.

"Nilimuarifu mtendaji aorodhoshe vitu wanavyokumbuka havipo ndani, ili waende kuripoti Polisi." Bwana Mwipi anasema.

Bado haijathibitishwa lengo la tukio hilo kufanyika, kwa kuwa hata humo ndani hakuna fedha zinazohifadhiwa humo. Aidha eneo hilo limekiri kutokuwepo na mikwruzo ya kidhini, na hivyo wanashangazwa na jambo hilo.

No comments:

Post a Comment