Watu wengi hawajui tofauti iliyopo kati ya mzimu ( Ghost ) na pepo ( Demon ). Tofauti ni hii hapa.
MZIMU NI NINI?
Zipo nadharia nyingi zinazo elezea mzimu ni kitu gani, nadharia iliyo zoeleka ni ile inayosema mzimu ni roho ya mtu aliye kwisha kufa. Mtu huyo anaweza kuwa amekufa zamani sana, ama muda mfupi ulio pita. Sitaizungumzia sana nadharia hii leo, isipokuwa nitazungumzia kwa ufupi nadharia nyingine inayo jibu mzimu ni kitu gani.
Mzimu ni nishati ( energy), roho au haiba ( personality) ya mtu ambaye amefariki dunia lakini imekwama katika sehemu iliyo kati ya duniani ( ulimwengu wa nyama/ulimwengu unao onekana ) na mahali ambapo roho hiyo inatakiwa kwenda kuishi baada ya maisha ya hapa duniani kukamilika ( ulimwengu usio onekana/ afterlife/ land of the souls )
. Watafiti wengi wana amini kuwa roho hizi zinakuwa hazijui kama zimekufa katika ulimwengu wa nyama ama hazitaki kuamini kama zimekufa katika ulimwengu wa nyama ama hazikubaliani na kifo chao katika ulimwengu wa nyama. Mara nyingi roho hizi huwa ni roho za watu ambao walikufa katika mazingira yanayo tatanisha kama vile kufa kwa kuuliwa bila sababu ( cold blood), kutolewa kafara, ama kufa baada ya maisha ya msukuleni. Kwa ufupi hizi huwa ni roho za watu ambao walidhulumiwa haki yao ya kuishi hapa duniani. Mizimu inaweza kujidhirisha na kuonwa na wanadamu ama wanyama katika namna tofauti tofauti kama vile muonekano ( hapa mizimu ,huwatokea ndugu, jamaa na marafiki zao wakiwa katika maumbo ya sura zao wakati wanaishi duniani na mara nyingi huwatokea wakiwa na nguo walizo penda kuzivaa wakati wa uhai wao ), sauti, harufu( hapa kwenye harufu mzimu unapo mtokea muhusika,hujidhihirisha kwa harufu yake ya mwili ( kila mtu ana harufu yake ya mwili, watu huweza kuwatambua watu wao wa karibu kwa harufu zao za mwili ), ama pafyumu ( katika pafyumu, mzimu utamtokea mtu kwa harufu ya marashi ambayo alikuwa anapenda kuyatumia wakati yupo duniani katika ulimwengu wa nyama. Wakati mwingine, mzimu huweza kuwatokea ndugu jamaa na marafiki zake kwa kuwashika.

Kwa ufupi mzimu huwa ni roho ambayo imewahi kuishi katika ulimwengu wa nyama kama mwanadamu ama mnyama.

PEPO ( DEMON ) Hawa ni roho waovu ambao hawajawahi kuwa wanadamu .Mara nyingi mapepo huwa na mitego mingi na huwa na tabia za kitoto kitoto sana ( Nitalizungumzia hili hapo baadaye ). Haiwezekani kuwazungumzia mapepo kwa parandesi moja pekee, hii ni kwa sababu kuna mambo mengi sana ambayo yanatakiwa kuzungumzwa kuhusu mapepo, maelezo ninayo yatoa hapa yanawazungumzia mapepo katika namna ambayo wanatofautiana na mizimu.

N.B: Mapepo ni wajanja sana, wakati mwingine huweza kuwatokea ndugu, jamaa, na marafiki wa mtu ambaye amekufa wakijifanya wao ndio roho wa mtu huyo na hivyo kuanza kutoa maelekezo ya kufanya kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu ambapo mwisho wa siku, wahusika wanajikuta wakiwa wamefungwa na nguvu za giza zitendazo kazi zake kutoka kuzimu. Ni muhimu sana kujua namna unavyo weza kutofautisha kati ya roho ya mtu aliyekuwa anaishi na roho za mapepo hawa ambazo huwatokea wahusika kwa ajili ya kuwadanganya..

TOFAUTI kubwa kati ya mizimu na mapepo ni kwamba, mizimu ni roho za watu ambao waliwahi kuishi hapa duniani kama binadamu ilihali mapepo ni roho ovu ambazo hazijawahi kuishi duniani kama wanadamu.
MASWALI MENGINE

1. Kuna aina ngapi za mizimu? ( Kuna mizimu mibaya na mizuri )
2. Mizimu inaishi wapi, inakula nini?
3. Mizimu ina nguvu kiasi gani na nguvu za mizimu zinaweza vipi kuwaathiri wanadamu?
4. Je wanyama kama mbuzi, mbwa, n’gombe, nyau, samba, chui, tembo n.k,. nao huwa wana mizimu?
5. Kati ya mizimu na mapepo nani mwenye nguvu kubwa kuliko mwenzake?

Kwa majibu ya maswali haya na mengine, tafadhali tembelea: ULIMWENGU USIONEKANA

Kama una swali lolote kuhusiana na masuala haya ya kiimani, tafadhali niandikie : mungwakabili@gmail.com

" MIMI NI MUNGU NIKUFUNDISHAYE ILI UPATE FAIDA........ISAYA 48;17 "