Pages

Tuesday 23 July 2013

WIZARA YAKIRI UBUYU NI DAWA

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imezungumzia utata uliopo kuhusu matumizi ya ubuyu ikisema sehemu kubwa ya mti huo hutumika kama dawa ya tiba za asili.


Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili na Mbadala kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Paulo Mhame alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu utata uliojitokeza kuhusu ubuyu katika semina iliyoandaliwa na wizara hiyo.

Kwa mujibu wa Dk. Mhame mti wa mbuyu hutumiwa na waganga wa tiba za asili kama dawa na sehemu kubwa inayotumika kama dawa ni majani, magome na unga wa ubuyu wenyewe.
“Lakini katika teknoloji zetu sisi Waafrika kusini ya Jangwa la Sahara hatuna namna ya kufanya mbegu kukamua, tunaweza kuikamua kwa kuisaga na kuitumia kama kiungo… Hii teknolojia ya kukamua mafuta ya karanga na kuisaga tumeiiga kutoka kwa wenzetu,” alisema Dk. Mhame.
Alisema katika kuzunguka kwake hajawahi kuona mahali wanapotumia mbegu kama dawa, kwahiyo hawezi kuzungumzia kama tiba asili lakini anaweza kuzungumzia matumizi ya ubuyu wenyewe kwa maana ya magome na unga wake na kwamba hafikiri kwamba matangazo yanayoendelea sasa yataathiri bidhaa hiyo.
Aliongeza kwamba pamoja na nchi kuiga teknolojia ya kukamua mafuta ya ubuyu kutoka kwa nchi za nje lakini hapa nchini kuna mashine mbili za kukamua mafuta ya ubuyu, akatolea mfano chache zilizopo mkoani Dodoma

No comments:

Post a Comment