Pages

Thursday, 25 July 2013

Cheka kidogo

Mama: Mwanangu hebu mpigie simu baba yako mwambie chakula tayari
Mtoto: Sawa mama
Mtoto: Mama simpati
Mama: Bac subir kama baada ya dakika tano mpigie tena inawezekana ni mambo ya network hayo.
(baada ya 5 mins)
Mtoto: Mama mimi baba simpati simu yenyewe anapokea mwanamke.
Mama: Kha! Sawa mwanangu niachie mm hili swala wewe nenda kale.
(baada ya 30mins)
Baba akabisha hodi akakaribishwa na bonge la kibao hajakaa vizur akapigwa sufuria mara mwiko ikawa balaa kwa kwenda mbele mme akazidiwa, majirani wakaja kuamulia ugomvi,kufika mme yuko chini ya sofa hoi bin taaban.
Mama"------- zako wewe, Kunifanyia mimi hivi unaenda kwa malaya zko kuniacha nyumbani?"
Mwanangu ebu wambie majirani yule mwanamke alipopokea simu alisemaje?
Mtoto: Alisema, "Samahani mteja wa nambari uliyopiga hapatikani kwa sasa"

No comments:

Post a Comment