Barua hii imeandikwa na kijana wa Kitanzania aliyekamatwa Hong Kong, China akijaribu kuingiza madawa ya kulenya nchini humo. “Punda wa Madawa/Drug Mule” ni mtu anayesafirisha madawa ya kulevya kwa kuyameza au kuyaficha sehemu fulani mwilini. Taarifa zisizo rasmi zinaonyesha kuwa Hong Kong pekee kuna wafungwa karibu 200 waliokamatwa kwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. 130 kati yao wameshahukumiwa na 70 bado wanangoja hukumu.
Kijana huyu ambaye ni mmoja kati vijana wengi wa Kitanzania waliokamatwa katika nchi mbalimbali, anaeleza ni jinsi gani Viongozi/Wanasiasa, Wafanyabiashara, Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Maafisa Usalama Viwanja vya Ndege, Uhamiaji na vyombo vingine vya usalama nchini vinahusika na biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment