Pages

Wednesday, 24 July 2013

Taifa Staz yatua Uganda jioni hii

Timu ya Taifa (Taifa Stars) inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imewasili Uganda jioni hii Jumatano tayari kuikabili Uganda Cranes kwa mechi ya marudiano kutafuta tiketi ya kucheza katika mashindano ya CHAN.
Kikosi hicho chichi nye wachezaji 20, kiliwasili muda mfupi baada ya saa kumi alasiri huku wachezaji na benchi la ufundi wakiwa na matumaini makubwa.
Akiongea mara baada ya kuwasili Kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen alisema wamejiandaa vizuri wakiwa Mwanza na ana imanikikosi hiki kitabadili matokeo ya awali ambapo Stars ilifungwa 1-0 na Cranes Jijini Dar es Salaam.
Alisema licha ya kuwakosa wachezaji Shomari kapombe na Mwinyi Kazimoto, ana imani na kikosi chake hiki kuwa kitafanya makubwa Kampala.

No comments:

Post a Comment