Pages

Friday, 26 July 2013

WINDOWS 7 YA KISWAHILI YAJA

Kwa kutambua umaarufu na umuhimu wa lugha ya Kiswahili duniani,Microsoft wametoa pack ya Kiswahili kwa ajili ya Widows 7 na Microsoft Office. Pack hii inapatikana online na zaidi ya yote ni BURE. Akizungumzia toleo hili boss wa Microsoft Afrika Mashariki na Kusini bwana Louis Otieno alisema
 

“zaidi ya watu million 150 wanaozungumza Kiswahili Afrika sasa wanaweza kuanza kutumia technolojia kwa lugha waipendayo na kuielewa zaidi. Hii ni mojawapo ya njia za kupanua wigo wa lugha duniani”.  
Viongozi na wabia mbalimbali Afrika na duniani kote wameipokea habari hii kwa furaha kubwa. Mkurugenzi wa elimu nchini Kenya mama Lydia Nzomo amesema Windows 7 ya Kiswahili ni ushindi kwa watoto wa shule za msingi kwani

itawasaidia kujua kutumia komputa haraka.
Microsoft wanasema toleo hili litahamasisha serikali za nchi husika kuongeza uwekezaji kwenye mambo ya IT, kupunguza ujinga na kuwavutia watu wengi zaidi kutumia komputa hasa kwenye nchi hizi ambazo utumiaji wa komputa bado ni mdogo.
 

Kazi ya kutengeneza toleo la Kiswahili lilifanywa na wataaluma wa lugha ya Kiswahili kutoka Afrika mashariki na kati kwa muda wa miaka miwili. Aliyeiongoza kazi hii ni mtafasiri wa lugha ya Kiswahili ndugu Mpasua Msonobari. Mpasua alisema kuna maneno zaidi ya 300,000 yliyotafasiriwa kwa Kiswahili kwenye toleo hilo jipya.
Download kwa kubonyeza hapa kupata toleo lako la Windows 7 toleo la Kiswahili
Microsoft wamekuwa wakishirikiana na nchi mbali mbali Afrika na duniani ili kuzitambua na kuzitafasiri lugha mbalimbali.

No comments:

Post a Comment