Pages

Tuesday, 30 July 2013

ORODHA YA TBS YA BIDHAA 48 ZISIZOTAKIWA KUONEKANA SOKONI...!!


 
 
Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI-- Shirika la Viwango (TBS) limetangaza orodha ya bidhaa 48 ambazo hazitakiwi kuwepo sokoni kutokana na muda wa kuitumia nembo ya kampuni hiyo katika bidhaa zao kumalizika na wahusika kushindwa kuwasilisha bidhaa zao kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuruhusiwa tena.

Hatua hiyo ya TBS inatokana na watengenezaji wa bidhaa hizo ambazo awali zilithibitishwa na TBS na kuruhusiwa kutumia nembo yao hiyo ya ubora kumalizika na wahusika kushindwa kuwasiliana na shirika hilo kwa ajili ya uhakiki wa bidhaa zao hizo .

Ofisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile aliliambia Mwananchi kuwa bidhaa hizo kuanzia hivi sasa hazitakiwi kuonekana sokoni na msako utaanza wakati wowote kuziondoa na zile ambazo zitakamatwa wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Tumetoa tangazo lakini kabla ya hapo tuliwapa muda wawe wameleta bidhaa zao kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kuruhusiwa kuendelea kutumia nembo yetu,akini wamekaidi ndio maana tumewatangazia kama utaratibu unavyoagiza” alisema Rhoida.

Bidhaa ziliazoainisha katika tangazo hilo ni pamoja na na
majina ya watengenezaji /wasambazaji katika mabano ni pamoja na karatasi laini ‘tissue’ za Alawi Supplies ya Zanzibar, Milk Marie Biscut za Britania, Maji ya Great Zone, Mishipi na nyavu za kuvulia samaki za Imara Fishnet, maji ya Raha na fulana za Kibo Trade.

Bidhaa zingine ni matofali ya GM Gross, taulo za watoto za Hengan Sanitary, baadhi ya rangi za Chui, beteri za Dry Cell, magodoro ya Jumbo foam, sabuni za Mbasira Investment ya Shinyanga, mifuko ya plastiki ya Centaza na mafuta ya kupikia ya Sun Flower Seed (Sun Shine) na korosho zinazosambazwa na Frabho Enterprises.

Pia taulo za wanawake za Sythentic Detergent (ARIEAL) za Procter&Gambler, mifuko ya B-Twill Jute na A-Twill, mifuko ya plastiki ya Tropical, mafuta ya kupikia ya Sun Flower ya A TO Z Oil Mills, Korosho za Munawar ya Mbeya, Sabuni za kunawia za Brite Chemicals, pipi, lawalawa, mipira ya kutafuna ya rangi mbili.

Vilainisha vya injini (Saud Oil) za Star Composed, betri za 777 kutoka China, maji ya kunywa ya Shia yanayotengenezwa na Siha Beverage, mtindi wa Morani Dairy ya Tanga, pikipiki za Star Shineray, vigae vya Mbezi, sabuni ya Liquid Detergent, mbao zilizotiwa dawa za Mombo, Jam iliyochanganywa ya Les Group ya Musoma.

Orodha hiyo pia inataja Jusi za nanasi za Unnat Fountain ya Morogoro, Maji Uluguru, springi za magari za kampuni ya TASIA, Gypsum zinazotengenezwa na Tanzania Gypsum ya Dar es Salaam, Maji ya Uzima, magodoro ya Plyfoam,Mvinyo wa nanasi wa Kivumbui ya Arusha na mabati ya RD Roofing & Wire Product.

Bidhaa zingine ni unga wa sembe wa Kweniml ya Machame Kilimanjaro, boriti za Ravji Manufacturing, mafuta ya breki za magari ya Automotive Packed ya Dar es Salaam, maJi ya kunywa ya AAMFA, pikipiki za Foshan Fost za China na mvinyo wa matunda wa Victoria Food Product ya Mara pia Jibini, mtindi na maziwa ya Kyaka Milk Processing , Sabuni za kufulia za Jamii za Kampuni ya Mbasira ya Shinyanga.
 



No comments:

Post a Comment