Pages

Tuesday, 23 July 2013

Wale wa Chigoma-Kibirizi

ENEO la Kibirizi lililopo mwambao wa ziwa Tanganyika katika
halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji huenda likageuka kuwa uwanja
... wa mapambano na umwagaji damu endapo hatua za haraka hazitachukuliwa
kutoka kwa mamlaka husika.

Hatua hiyo inafuatia uongozi wa Manispaa hiyo kutoa zabuni za ujenzi
wa gati na Bandari katika eneo hilo huku baadhi ya wananchi wakidai kuwa hawana taarifa juu ya mradi huo huku wengine wanadai malipo ya fidia baada ya kufanyiwa tathimini ya malipo wanayostahili.

Ni miti aina ya Michikichiki inayozalisha mawese ambayo ni maarufu kwa
uchumi wa manispaa ya Kigoma Ujiji na taifa kwa ujumla lakini ujenzi
wa bandari mpya unatishia uwepo wake baada ya kuanza kukatwa bila
wamiliki kupewa fidia hatua inayofanya baadhi ya wahanga kulalamikia
hali hiyo .

Kibirizi ni tegemeo kubwa kwa raia wa nchi jirani za Burundi, Congo
DRC na Zambia kupitia ziwa Tanganyika ambao huja nchini kuhemea
mahitaji mbalimbali na kutoa fedha ambazo husaidia kuinua hali za
kiuchumi kwenye familia zenye kipato kidogo.

Ukosefu wa taarifa sahihi na elimu ya kutosha ni kikwazo kinachoweza
kukwamisha kukamilika kwa ujenzi wa gati hilo kutokana na
ushirikishwaji mbovu wa viongozi wa ngazi za chini huku utashi wa
kisiasa ukitajwa kuchangia.

Takribani wiki moja iliyopita kituo cha televisioni cha Star tv kimeripoti kuhusu wakazi hao
zaidi ya 800 kulalamikia hatua ya Manispaa ya Kigoma Ujiji
kuwasainisha fomu za malipo bila kujua thamani halisi ya pesa zao na
hivyo kuibua mgogoro mpya kati yake na wananchi.

No comments:

Post a Comment