BARUA YENYEWE INASOMEKA KAMA IFUATATAVYO:
MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania
YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.
Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa
heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU
ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na
jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa
njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha
maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.
Mh.Rais
mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa
natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono
yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki
Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)
No comments:
Post a Comment