WIZARA ya Afya na Ustawi
wa Jamii imezungumzia utata uliopo kuhusu matumizi ya ubuyu ikisema
sehemu kubwa ya mti huo hutumika kama dawa ya tiba za asili.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili na Mbadala kutoka Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk. Paulo Mhame alisema hayo jana jijini Dar es
Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu utata
uliojitokeza kuhusu ubuyu katika semina iliyoandaliwa na wizara hiyo.
Kwa mujibu wa Dk. Mhame
mti wa mbuyu hutumiwa na waganga wa tiba za asili kama dawa na sehemu
kubwa inayotumika kama dawa ni majani, magome na unga wa ubuyu wenyewe.
“Lakini katika teknoloji
zetu sisi Waafrika kusini ya Jangwa la Sahara hatuna namna ya kufanya
mbegu kukamua, tunaweza kuikamua kwa kuisaga na kuitumia kama kiungo…
Hii teknolojia ya kukamua mafuta ya karanga na kuisaga tumeiiga kutoka
kwa wenzetu,” alisema Dk. Mhame.
Alisema katika kuzunguka
kwake hajawahi kuona mahali wanapotumia mbegu kama dawa, kwahiyo hawezi
kuzungumzia kama tiba asili lakini anaweza kuzungumzia matumizi ya
ubuyu wenyewe kwa maana ya magome na unga wake na kwamba hafikiri kwamba
matangazo yanayoendelea sasa yataathiri bidhaa hiyo.
Aliongeza kwamba pamoja
na nchi kuiga teknolojia ya kukamua mafuta ya ubuyu kutoka kwa nchi za
nje lakini hapa nchini kuna mashine mbili za kukamua mafuta ya ubuyu,
akatolea mfano chache zilizopo mkoani Dodoma
No comments:
Post a Comment